Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, manaibu wa uongozi wa Hawza ya Mkoa wa Hormozgan Iran, pamoja na wakurugenzi wa shule za mkoa huo walikutana na Ayatullah Muhammad Mahdi Shabzendehdar, Katibu wa Baraza Kuu la Hawza.
Ayatullah Shabzendehdar, akizungumzia mazingira ya kipekee ya Hawza ya Mkoa wa Hormozgan, alisema: “Ninyi mnafanya kazi katika mazingira ambayo, kwa upande mmoja, ni mkoa wenye mchanganyiko wa kimadhehebu, na kwa upande mwingine, kwa sasa uko katika hali ya vita. Na kwa hakika, ‘Matendo bora zaidi ni yale yaliyo magumu zaidi.’”
Akifafanua kwamba Mwenyezi Mungu ametaja katika sehemu tatu za Qur’ani Tukufu kuwa lengo la kumuumba mwanadamu ni kumjaribu ili kubaini ni nani miongoni mwao anayefanya matendo kwa ubora zaidi (Ahsan Amalan), alisema: “Hapa kuna mjadala wa tafsiri ya Qur’ani, kwamba je, kinachokusudiwa ni kila tendo na kitendo kuchunguzwa kivyake ili kubaini kama ni bora zaidi au la, au kinachokusudiwa ni wastani wa utendaji wa mtu katika kipindi chote cha maisha yake kuwa bora zaidi?”
Katibu wa Baraza Kuu la Hawza aliongeza kwamba; kila mtu anapaswa kuweka dhamiri na itikadi yake katika msingi wa kuhakikisha kwamba, katika tathmini na maamuzi anayoyafanya, anaelekeza juhudi zake zote katika kufikia kiwango ambacho, tendo lake linapolinganishwa na matendo ya watu wengine, anastahili kutunukiwa nishani ya Ahsan Amalan na Mwenyezi Mungu.
Akirejelea hadithi kutoka kwa Imam Sadiq (as), iliyonukuliwa katika kitabu Al-Kafi, Juzuu ya Pili, ukurasa wa 81, alisema kwamba; hadithi hiyo inaeleza kuwa kipimo cha kufanya matendo kwa ubora zaidi si wingi wa matendo, bali ni kiwango ambacho matendo hayo yanaendana na maadili na misingi inayokubalika.
Alielezea kumcha Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu na utambuzi wa ukuu Wake, kuwa nguzo ya kwanza ya kufanya matendo kwa ubora zaidi kwa mujibu wa hadithi hiyo. Akifafanua tofauti kati ya khawf na khashyat, alisema: “Khawf maana yake ni hofu, yaani mtu anaogopa kwamba wakati wa kuhesabiwa matendo yake atakuwa miongoni mwa watu wa Jahannamu na Moto. Bila shaka, hofu hiyo pia ni jambo linalotakiwa. Hata hivyo, khashyat hutokana na maarifa ya juu kuhusu Mwenyezi Mungu. Kupitia maarifa hayo ya juu, mtu hujawa na unyenyekevu mbele ya utukufu wa Mola wake, hata kama ni Maasumu na hakuna dhambi yoyote inayotoka kwake.”
Mwanazuoni huyo wa Hawza ya Qum alitaja sababu ya pili kuwa ni nia njema ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, akibainisha kwamba ikiwa kiongozi atakuwa na khashyat ya Mwenyezi Mungu, basi matendo na maamuzi yake yatatekelezwa kwa kuzingatia msingi huo muhimu.
Akizungumza na walimu wa Hawza, alisema: “Ikiwa mwalimu anataka kuwa miongoni mwa waliofanya matendo kwa ubora zaidi, anapaswa kuwajali wanafunzi wa Hawza, kusoma na kujiandaa vizuri, kuwasilisha masomo kwa namna bora, kuwa na nidhamu, kufika kwa wakati na kuwa na maadili ya kiroho.”
Mjumbe wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qum, akirejelea mifano ya maadili ya kiroho na kuzingatia masuala ya kujitakasa kimaadili miongoni mwa wanazuoni wakubwa na watangulizi wa Hawza, alisema kwamba mwalimu anapokuwa na maadili ya kiroho, mwanafunzi hunufaika kwa njia mbili: hujifunza masomo yake na pia hunufaika na maadili ya kiroho ya mwalimu wake.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, akimzungumzia marehemu Ayatullah Sayyid Musa Shubairi Zanjani, alitaja umakini na uimara katika tafiti za kielimu, pamoja na unyenyekevu na kujishusha, kuwa miongoni mwa sifa za mwanazuoni huyo aliyekuwa Marjaa wa Taqlidi. Pia, alieleza kwamba kifo chake kimekuwa pigo kubwa.
Ayatullah Shabzendehdar alitaja ikhlasi kuwa miongoni mwa sifa kuu zilizomtofautisha Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, kama ilivyokuwa kwa Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu awarehemu wote wawili). Alieleza kwamba mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu yalitokana na ikhlasi hiyo, akisema: “Ikhlasi hii ilileta baraka ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuyawezesha kusimama imara mbele ya matatizo yote yaliyosababishwa na maadui.”
Maoni yako